Lydia Mollel – Morogoro.

Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro, linamshikilia mtu mmoja Selemani Sita (25), mwenyeji wa Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya Mwanamke mmoja Mwanaisha Matere (37), na Mtoto wake Baraka Maita (7), kwa kuchinjwa shingo na kutenganishwa viwiliwili vyao.

Mauaji hayo, yametekelezwa katika kitongoji cha ILangali, kilichopo kata ya Mililani Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro usiku wa kuamkia November 24,2023 ambapo mtuhumiwa huyo alipewa hifadhi ya muda, akihudumu kama Msaidizi wa Shambani.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema uchunguzi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuatwe.

Hata hivyo, amesema jamii inatakiwa kuacha tabia ya kupokea wageni wasiowafahamu na badala yake watoe taarifa za ugeni wowote katika ofisi za Serikali za mitaa yao ambapo wakati wa tukio hilo, inadaiwa kuwa Baba wa Familia hiyo alikuwa amesafiri.

Agizo la Waziri Mkuu lawasilishwa kwa Wakurugenzi
Wolves kumng'oa Aaron Ramsdale Arsenal