Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 23, 2022 ameshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi katika Makazi yake ya Kijiji cha Nandagala, kilichopo Ruangwa Mkoani Lindi.

Akizungumza baada ya kuhesabiwa, Majaliwa ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kuhesabiwa na kutoa taarifa kwa makarani wa Sensa ili taarifa hizo ziweze kutumika katika kupanga mipango ya maendeleo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwakaribisha makarani wa Sensa nyumbani kwake Kijijini Nandagala – Ruangwa Mkoani Lindi.

Aidha Majaliwa amesema kuwa zoezi la sensa litaiwezesha Tanzania na Watanzania kushiriki kwa pamoja mipango ya dunia sambamba na mashirika mbalimbali ya kimataifa katika shughuli za kujiinua kiuchumi.

Amesema “Mashirika haya yakijua tupo wangapi yatakuwa na nafasi kubwa ya kujua namna ya kutusaidia na hii ni kwa Watanzania wote nawasihi kwa pamoja tujitokeze tuhesabiwe na taarifa hizi ziwe msaada kwa Taifa”

Sensa: Tulia awatoa hofu Watanzania maswali ya Makarani
Zalan FC kucheza KWA MKAPA