Watu 12 wamefariki na wengine 63 kujeruhiwa, katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia hii leo Februari 9, 2023 katika Kijiji cha Silwa kilichopo Kata ya Pandambili Wilayani Kongwa, barabara kuu ya Dodoma – Morogoro Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema ajali hiyo imehusisha Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 677 DVX na basi la abiria Kampuni ya Frester lenye namba za usajili T 415 DPP lililokuwa likitokea Bukoba kwenda Dar es Salaam.

Amesema, waliofariki katika ajali hiyoni wanaume wanane na wanawake wanne huku majeruhi wakiwa ni wanaume 40 na wanawake 23 ambao wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa na Kituo cha Afya Gairo.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mkoa wa Morogoro na majeruhi 2 wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma huku Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Awadh Haji akitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi kutaka kulipita gari la mbele bila ya kuchukua tahadhari.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwajulia hali majeruhi waliolazwa katika Kituo cha Afya Gairo.

Ajali ya Basi na Lori: Miili 11 yahifadhiwa Hospitali Morogoro
European Super League yajimwambafai