Miili ya marehemu 11 kati ya 12 ya watu waliofariki katika ajali ya Basi kugongana na Lori usiku wa kuamkia hii leo Februari 9, 2023 eneo la Kijiji cha Msilwa kilichopo Pandambili Mkoani Dodoma, imepokelewa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro

Kati ya waliofariki kwenye ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Silwa Pandambili Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ni Askari Polisi Koplo Hamisi huku Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro Dkt. Kessy Ngalawa amethibitisha kupokea miili hiyo.

Dar24 Media imezungumza na mmoja wa ndugu wa Marehemu Koplo Hamis ambaye amejitambulisha kwa jina la Hamis Issa na kusema ndugu yake alikuwa anafanya kazi Mkoa wa Kipolisi Ilala na ajali imempata wakati akitoka kumchukua mtuhumiwa.

Ajali hiyo, imehusisha Basi la abiria la kampuni ya Frester lililokuwa likitoka Bukoba kwenda Dar Es Salaam kugongana uso kwa uso na Lori majira ya saa sita usiku iliyotokea Barabara kuu ya Dodoma Morogoro.

Udanganyifu hauna namna ya kuutetea: Spika Dkt. Tulia
Senyamule awajulia hali majeruhi ajali ya Basi la Lori Dodoma