Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema udanganyifu hauna namna ya kuutetea na kwamba Viongozi wana jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa Kielimu na kitaaluma.

Dkt. Tulia ameyasema hayo hii leo Februari 9, 2023 Bungeni jijini Dodoma, na kusema Serikali inatakiwa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa wale wanaosababisha uwepo wa wale wanaohusika kwenye udanganyifu.

Amesema, “Hakuna namna ya kuutetea udanyanyifu na haupaswi kabisa kuvumilika kwasababu mwisho wa haya hawa ndio wanaokuja kuchukua nafasi zote tulizonazo maana mwanafunzi hawezi kuwa na mtihani kama hakuwezeshwa kuwa na mtihani na ndio maana tunasema wachukuliwe hatua.”

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

Kuhusu Shahada za heshima, Spika Tulia amesema anapopewa Rais huwa imefanywa tafiti ya kina ya kazi alizozifanya sio kwa nafasi aliyonayo kama Rais bali tangu alipoanza kufanya kazi na anakuwa tofauti na wale waliolipa pesa ili wapewe.

Amesema “sisi kama Taifa, ni lazima kufahamu ni utaratibu upi tunapaswa kwenda nao kwasababu tusipofanya hivyo tunajipoteza wenyewe, na sisi kama viongozi ni lazima tuoneshe mfano, mtoto wako unampeleka shule unalipa pesa ili apate elimu, leo wewe kama mzazi unalipa pesa ili upewe degree unampa mfano gani kijana unayemkzania kusoma?.”

Aidha tulia ambaye alikuwa akifafanua kuhusu utaratibu wa utoaji wa Shahada wa vyuo vinavyotambuliwa na visivyotambuliwa, amesema ni vyema wao kama viongozi na pia kama Taifa kuweka muongozo mwema kwa ajili ya wale wanaowafuata nyuma.

Tetemeko la ardhi latikisa Tanzania, Kenya
Ajali ya Basi na Lori: Miili 11 yahifadhiwa Hospitali Morogoro