Watu 12 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha Basi la abiria la kampuni ya Frester, lililokuwa likitoka Bukoba kuelekea Mkoani Dar es Salaam na Lori lenye tela aina ya Scania, lililokuwa limebeba saruji.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wamesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 katika Kijiji Cha Silwa, kilichopo Pandambili Wilayani Kongwa barabara kuu ya Dodoma – Morogoro.

Wamesema, chanzo cha ajali na magari hayo kugongana uso kwa uso ni baada ya dereva wa basi hilo la Frester lenye namba za usajili Tkutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake, bila kuchukua tahadhari.

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na ameongeza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule yuko eneo la tukio na juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma zinaendelea ili kuweza kuthibitisha na kupata taarifa kamili.

Simba SC yataja sababu za Saido kubaki Dar
Serikali yaangazia unafuu mfumuko wa bei