Klabu ya Inter Miami imethibitisha kumsajili mchezaji huru Sergio Busquets baada ya kumaliza mkataba wake na Mabingwa wa Soka nchini Hispania FC Barcelona.

Busquets alitumia misimu 15 katika kikosi cha kwanza cha Barca kabla ya kuondoka mwishoni mwa Juni mwaka huu, na kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, saba ya Copa del Rey na tisa ya Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ likiwamo moja la mwaka wake wa mwisho katika klabu hiyo wakati wa maisha yake ya soka.

Kiungo huyo wa kati sasa ameungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barca, Lionel Messi huko Miami.

Akizungumza baada ya kuhamia huko, kupitia tovuti rasmi ya klabu, Busquets alisema: “Hii ni fursa maalum na ya kusisimua ambayo ninafurahia sana kuichukua. Natarajia hatua hii inayofuata katika kazi yangu na Inter Miami.

“Nilifurahishwa na klabu nilipokuja na FC Barcelona mwaka jana na sasa nina furaha na niko tayari kuwakilisha klabu mwenyewe. Siwezi kusubiri kusaidia kuleta mafanikio ambayo klabu hii kabambe inapigania.”

Mmiliki Mkuu wa Inter Miami, Jorge Mas pia alielezea furaha yake kupata mkataba huo: “Nina furaha kumkaribisha Sergio Busquets hapa Inter Miami. Tangu siku ya kwanza tumedhamiria kuleta wachezaji bora duniani Inter Miami. Sasa ripoti inajieleza yenyewe.”

Mzee Chasamba atoboa siri Mwl. Nyerere alivyompa Ukamanda
Habibu Kondo kocha mpya Mtibwa Sugar