Kwa mara ya kwanza mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Kun Aguero amekanusha taarifa za kuwa mbioni kuihama Man City kwa kisingizio cha kuchoshwa na falsafa za meneja mpya wa klabu hiyo Pep Guardiola.

Aguero amekanusha uvumi huo akiwa katika kambi ya kikosi cha timu ya taifa lake la Argentina, ambapo amesema hakuwahi kufikiria jambo kama hilo, na ameshangazwa kuona na kusikia taarifa za kutaka kuondoka Man City.

Amesema kinachoendelea katika vyombo vya habari ni uzushi ambao hauna chembe ya ukweli, na anaamini huenda kuna baadhi ya watu wanatoa msukumo wa jambo hilo ili kufahamu nini atakachokifanya mwishoni mwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo ambaye ni baba mkwe wa gwiji wa soka nchini Argentina Diego Armando Maradona, amesema tangu Pep Guardiola alipowasili Etihad Stadium wamekua na uhusiano mzuri na mara kadhaa hushauriana mambo mengi ya kimsingi kuhusu Man City.

Kuhusu suala la kushindwa kucheza katika kikosi cha kwanza kwa zaidi ya mara nne Aguero amedai kuwa, utakua upuuzi kwa mtu kama yeye ambaye amekomaa katika soka la kimataifa kuingilia kazi ya meneja ambaye anapaswa kufahamu nani anastahili kuanza kwenye kikosi chake.

“Soka ni mchezo wa mipango, na kazi hiyo siku zote hufanywa na meneja, siwezi kuingilia na kulazimisha nianzishwe katika kikosi cha kwanza,” Alisema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 wakati akifanyiwa mahojiano na ESPN Radio.

“Labda kuna jambo ambalo watu wengi hawalifahamu, mimi na Guaradiola tuna ukaribu mkubwa sana na amenisaida sana katika maendeleo ya soka langu, sasa iweje tunataka kuchonganishwa kwa maslahi ya vyombo vya habari?” alihoji Aguero.

Stefano Pioli Adhihirisha Mahaba Yake Inter Milan
Juan Antonio Pizzi: Sanchez Atacheza Dhidi Ya Man Utd