Nahodha na beki wa klabu ya Real Madrid, Sergio Ramos, itamlazimu kusubiri hadi kumalizika kwa mchezo wa mahasimu wakubwa nchini Hispania, ndipo afanyiwe upasuaji wa bega.

Ramos, alitonesha maumivu wa bega wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Real Madrid walikubali kichapo cha mabao matatu kwa mawili kutoka kwa Sevilla.

Vipimo vya awali ambavyo amefanyiwa beki huyo mwenye umri wa miaka 29, vinaonyesha anaweza kusubiri hadi mchezo dhidi ya FC Barcelona ukapita, na ndipo shughuli nyingine za kitabibu zichukua mkondo wake.

Benchi la ufundi la klabu ya Real Madrid, limeutazama uwezekano huo kwa kuomba msaada katika jopo la madaktari, hali ambayo ilionyesha kuzaa matunda, kutokana na uzito wa mchezo wa novemba 21 ambapo FC Barcelona, watasafiri kuelekea Estadio Stantiago Bernabeu mjini Madrid.

Ramos, alipata maumivu wa bega kwa mara ya kwanza, septemba 15, wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk, lakini bado alionekana anaweza kuendelea kupambana katika michezo iliyofuatia.

Hata hivyo pamoja na yote hayo, iwe isiwe Ramos hatoweza kukikwepa kisu, mara baada ya mchezo wa novemba 21 dhidi ya FC Barcelona, ili kunusuru hali yake kiafya.

Memphis Depay Arudisha Ujumbe Kwa Mashabiki
Utafiti: Sababu Za Wanaume Wasio Na Fedha Kuwapenda Wanawake Wenye Maumbo Haya