Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema Serikali imefanya utafiti kuhusu teknolojia mbadala wa zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini.

Khamis ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya hatua zilizofikiwa juu ya uratibu na utekelezaji wa Mpango-kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki (2020 – 2025) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya hatua zilizofikiwa juu ya uratibu na utekelezaji wa Mpango-kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki (2020 – 2025) iliyowqasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma Agosti 22, 2023.

Amesema, utafiti umeonesha teknolojia za kuchoma (smelting) kwa kutumia borax na teknolojia za sianadi ndio zinatumika kwa wingi nchini na nchi zinazoendeleana na kwamba Mradi wa Kudhibiti Athari za Zebaki kwa Afya ya Binadamu na Mazingira Kwenye Shughuli za Uchimbaji Mdogo wa Dhahabu Nchini, umejikita katika kufanyia kazi teknolojia zinazotumika zaidi nchini.

”Lengo ni kutekeleza malengo la Mkataba wa Minamata hususan kipengele cha saba kinachohusu kupunguza matumizi ya zebaki kwenye uzalishaji wa dhahabu inayozalishwa na wachimbaji wadogo na pale itakapowezekana kuondoa kabisa matumizi ya kemikali hiyo katika kuzalisha dhahabu kwa wachimbaji wadogo,” alifafanua Naibu Waziri huyo.

Ali Ramathan Mwirusi asaini dili Hispania
Mwakinyo kuwania ubingwa IBA Dar