Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuimarisha na kuweka mazingira mazuri wezeshi ya kibiashara katika uwekezaji nchini.

Rais Mwinyi ameyasema hayo hii leo Machi 10, 2023 wakati akizindua Muongozo wa Uwekezaji na Mfumo wa Kieletroniki wa Uwekezaji (ZIPA).

Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji na Mfumo wa Kieletroniki wa Uwekezaji (ZIPA).

Mwongozo huo una madhumuni ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wawekezaji ikiwemo usajili na upatikanaji wa cheti cha uwekezaji wenye jina la”Zanzibar Investment Electronic Window” (ZieW).

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia amesema suala la kukuza uwekezaji ni moja ya malengo makuu ya Serikalina ya kuleta Maendeleo nchini.

Dkt. Yonazi azungumza na Menejimenti ya Tume TACAIDS
Kampuni ya Yutong kufungua Karakana nchini