Serikali nchini Afrika Kusini, imefikia makubaliano ya kuhamisha zaidi ya Duma 100 kwenda nchini India, kama sehemu ya mradi wa kurudisha mnyama huyo mwenye madoadoa.
Wizara ya mazingira ya Afrika Kusini, imesema kundi la kwanza la duma 12 litasafirishwa hadi India mwezi ujao, kuungana na wengine wanane walioagizwa kutoka Namibia Septemba, 2022.
Taarifa ya Wizara hiyo imeeleza kuwa, “mpango ni kuhamisha duma wengine kumi na wawili kila mwaka katika kipindi cha miaka 8 hadi 10, ili kusaidia kuongeza idadi ya duma wanaoweza kuishi kwa amani na salama.”
Nchi ya India, iliwahi kuwa na duma wa kutoa Asia, spishi ndogo iliyotangazwa kutoweka mwaka wa 1952 baada ya kukosa makazi yanayofaa na kutokana wawindaji kuwauwa ili kupata ngozi yake kwa matumizi ya kibinadamu.