Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema Tanzania itaanza kuhifadhi akiba ya mafuta yatakayotumika katika kipindi cha zaidi ya miezi mitatu, tofauti na sasa ambapo inahifadhi kwa mujibu wa sheria kwa siku 15 pekee.

Makamba ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika hafla ya uwekaji saini hati ya makubaliano kati ya Wizara ya Nishati na Kampuni ya Mafuta toka Falme za Kiarabu, Erikali.

Amesema, ujio wa kampuni hiyo utasaidia kuboresha miundombinu ya bomba la kushusha mafuta bandarini na uhifadhi wa mafuta ya kutosha nchini.

Upungufu wa mafuta Duniani umesababishwa na mambo mengi ikiwemo bei za mafuta katika soko la dunia, kuongezeka kwa kiwango kikubwa kuanzia Februari 2022 na bei za hitaji hilo zilianza kuongezeka Januari 2022 baada ya uwepo wa vita.

Njia ya kumpata mtoto wa jinsia unayotaka
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 28, 2023