Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF limetoa wito wa kuachiliwa kwa watoto 13, wavulana 11 na wasichana 2, waliotekwa nyara mapema wiki hii mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati wa shambulio lililohusishwa na waasi wa Uganda wa Allied Democratic Forces, ADF.

Shambulio hilo lililotokea katika kijiji cha Makugwe katika mkoa wa Kivu Kaskazini liliua takriban watu 24 usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu Januari 23-24, 2023.

Wanajeshi wa DRC wakivuka barabara inayoelekea mji wa Beni hadi mpaka wa Uganda. Picha ya AFP.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF limesema katika shambulio hilo watu 24 waliuawa, ikiwa ni pamoja na msichana mwenye umri wa miaka 13 na wanawake watano na watoto saba wenye umri wa miaka 9 hadi 12, walitenganishwa na wazazi wao.

ADF, waasi wa Kiislamu wenye asili ya Uganda, wanaendesha harakati zao kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini na Kusini mwa mkoa jirani wa Ituri, ni moja ya makundi mabaya zaidi ya watu wenye silaha katika eneo la mashariki mwa DRC na limedai kuhusika na tukio hilo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 28, 2023
Matukio dawa za kulevya, ulawiti yashamiri Tanga