Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameshiriki zoezi la usafi huko Mbagala Wilayani Temeke na kupiga marufuku ufanyaji wa Biashara kwenye ujenzi wa Barabara ya mwendokasi na maeneo yaliyokatazwa.

Makalla, ambaye ameyasema hayo hii leo Januari 28, 2023 pia ametumia zoezi hilo kuwakumbusha Wananchi na Viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi Wilaya, kuhakikisha wanasimamia usafi Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla akiongea mara baada ya zoezi hilo la ufanyaji wa usafi.

Aidha, RC amewaelekeza Wakurugenzi kusimamia Wakandarasi kuondosha taka kwa wakati na wale watakaolega wasipatiwe mkataba mpya hukiu akiwapongeza Wananchi kwa mwamko usafi jambo lililopelekea Dar es salaam kushika nafasi ya sita kwa usafi Barani Afrika, na kuondosha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam amesema zaidi ya shilingi bilioni 3.2 zimetolewa kama mkopo kwa Wafanyabiashara wa maeneo rasmi na hivyo kutoa wito wa kuacha kufanya biashara kiholela.

Serikali kusafirisha Duma 100 nje ya nchi
Randy Bangala mambo safi Dodoma Jiji