Uongozi wa Dodoma Jiji FC umekamilisha vibali vyote vya nyota wake kutoka DR Congo Randy Bangala, ambaye hakuwahi kuitumikia klabu hiyo tangu aliposajiliwa mwanzoni mwa msimu huu.

Randy ambaye ni mdogo wake Yannick Bangala wa Young Africans alisajiliwa Dodoma Jiji FC Julai 7-2022, akitokea timu ya AS Maniema Union ya DR Congo.

Akizungumza suala la kiungo huyo katibu mkuu wa Dodoma Jiji FC Fortunatus Johnson amesema, kila kitu kimekamilika na wanaamini wataanza kumuona Randy akicheza.

Amesema jukumu lililopo kwa sasa ni la Benchi la Ufundi kumtumia mchezaji huyo, kwa ajili ya kuisaidia timu katika Michuano ya Ligi Kuu, baada ya kutolewa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kwa kufungwa na Azam FC 4-1.

“Shida ilikuwa ni kupata kibali chake cha uhamisho wa kimataifa (ITC), katika klabu aliyotokea ya Maniema Union hivyo tunashukuru kwani kila kitu kipo sawa,”

“Kwa sasa kila kitu kimeenda vizuri, tunaamini Benchi la ufundi litaanza kumtumia katika michezo yetu ya Ligi Kuu, ili aisaidie timu yetu kumaliza kwenye nafasi nzuri katika msimamo.” amesema Fortunatus.

Makalla apiga marufuku biashara maeneo ya ujenzi Mwendokasi
Chongolo ataka tamati ya migogoro Wakulima na Wafugaji