Serikali ya nchi ya Zimbabwe, imeanza kuwahamisha zaidi ya wanyama pori 2,500 kutoka hifadhi ya kusini kwenda kaskazini mwa nchi hiyo ili kuwaokoa na ukame, huku uharibifu wa mabadiliko ya tabianchi ukichukua nafasi ya ujangili kama tishio kwa wanyamapori.
Takriban tembo 400, pala 2,000, twiga 70, nyati 50, nyumbu 50, pundamilia 50, nyanda 50, simba 10 na kundi la mbwa mwitu 10 ni miongoni mwa wanyama wanaohamishwa kutoka Hifadhi ya Bonde la Save Valley ya Zimbabwe kwenda kwenye hifadhi tatu.
Sapi, Matusadonha, na Chizarira ni moja kati ya mazoezi makubwa zaidi ya kukamata wanyama hai na kuwahamisha kusini mwa Afrika, uliopewa jina la “Project Rewild Zambezi,” lililenga kuhamisha wanyama kwenye eneo la bonde la Mto Zambezi ili kujenga upya idadi ya wanyamapori katika eneo hilo.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60, tangu Zimbabwe kuanza harakati za ndani za wanyamapori ambapo kati ya mwaka 1958 na 1964, nchi hiyo ilipokuwa ikiitwa Rhodesia, zaidi ya wanyama 5,000 walihamishwa katika zoezi lililoitwa “Operesheni Nuhu.”
Operesheni hiyo, iliokoa wanyamapori kuondokana na hatari ya kuongezeka kwa maji yaliyosababishwa na ujenzi wa bwawa kubwa la umeme kwenye Mto Zambezi, ambalo liliunda moja ya maziwa makubwa zaidi ulimwenguni, likiitwa Kariba.