Serikali imepiga marufuku uvutaji wa shisha nchini kutokana na madhara yake pamoja uwepo wa wimbi kubwa la watu hususan vijana wanaotumia.

Marufuku hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa amehudhuria hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na madhehebu ya Shia jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Waziri Mkuu alieleza kuwa Shisha ambayo hutumia tumbaku huchanganywa pia na vilevi vingine haramu na kusababisha upotevu wa nguvu kazi ya taifa.

Agizo hilo la Waziri Mkuu limekuja siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza kupiga marufuku uvutaji shisha, uvutaji sigara katika maeneo ya wazi pamoja na vitendo vya ushoga.

Makonda alieleza kuwa amebaini kuwepo kwa taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zilizopokea pesa nyingi kutoka ughaibuni kwa lengo la kufadhili vitendo vya ushoga na akaahidi kuifuta. Pia, alipiga marufuku watu kuwafollow mashoga wanaojitangaza katika mitandao ya kijamii.

Katika Afrika Mashairiki, mwaka jana Bunge la Uganda lilipisha sheria mpya ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku ambapo iliharamisha uvutaji ‘Shisha’. Huenda Tanzania pia ikalazimika kuandaa muswada wa kuyaweka makatazo hayo katika sheria.

Video: Mtazame mchezaji Musa Saidi wa Tanzania akipasha huko Ufaransa, COPA Camp ya 2016
Lowassa adaiwa kujipanga kung’oka Chadema..!