Serikali ya Wilaya ya Moshi imelifunga kwa muda Kanisa la Evangelist Asembles of God (E.A.G.T), Mawenzi kutokana na mgogoro kati ya waumini na uongozi wa juu wa Kanisa

Chanzo cha mgogoro inadaiwa kuwa uongozi wa juu wa Kanisa hilo ulichukua uamuzi wa kumuondoa Mchungaji Mwanzilishi wa Kanisa hilo katika mtaa huo, Frank Mushi na kumleta Mchungaji mwingine pasi na ridhaa ya waumini.

Uongozi wa Kanisa umesema sababu ya kumuondoa Mchungaji huyo ni kutokuwa na Elimu ya Dini (Theology), hivyo hajakidhi vigezo vya kutoa huduma kwa waumini.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo amesema, kuwa uongozi wa kanisa ulikimbilia polisi, badala ya kumaliza mgogoro huo ndani ya Kanisa kwa sababu wanataka kutumia nguvu kuleta Mchungaji mpya na kumuondoa yule aliyekuwepo.

Wakati Mchungaji Frank Mushi anafukuzwa alikuwa tayari amepanda ngazi ya uongozi na kufikia kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Kilimanjaro.

Mambo yamgeukia Gervinho, apigwa marufuku
Lionel Messi ajibu tuhuma za Eric Abidal