Serikali ya Libya inadaiwa kujaribu kukanusha vitendo vya mateso na ubakaji dhidi ya wahamiaji vilivyokuwa vikifanyika nchini humo bila ya kuwaadhibu wahusika wa matukio hayo yaliyolalamikiwa na mashirika kadhaa ya Haki za binadamu.

Mmoja wa watafuta hifadhi kutoka eneo la Daraa nchini Syria, Mohamed Noor amesema hali hiyo iliyowakumba watu kadhaa, haionekani kubadilika tangu wakati huo, huku madai ya kuwatendea vibaya wahamiaji walio kizuizini, yamekuwa yakipuuzwa.

Amesema, “Sasa mguu wangu umeumia sana maana nililazimika kuogelea kutoka kwenye boti ya Zawiya, sikuweza kujua kilichotokea baadaye kwani walinzi wa pwani na wanamgambo wa Libya, wale ni wahalifu walitufanyia vitendo vya kikatili sana.”

Wahamiaji waliookolewa wakiwa wameketi karibu na mashua ya Walinzi wa Pwani katika mji wa Khoms, takriban kilomita 120 (maili 75), mashariki mwa Tripoli, Libya. Picha na Hazem Ahmed/AP.

Amesema, walinzi hao na wanamgambo ni wangeweza kuwauwa kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa wasamaria wema kuwa mwaka jana waliona watu wakiuawa na walinzi wa pwani wa Libya, wakiwemo watu wanane kutoka mataifa ya Afrika.

Licha ya malalamiko ya mara kwa mara, lakini maelezo ambayo hayajathibitishwa yanasema vifo vya wahamiaji, vimekuwa havitambuliki au kunyamaziwa na Umoja wa Ulaya unaonekana kuziba masikio na unaendelea kushirikiana na Serikali ya mjini Tripoli.

Mapema mwezi Agosti 2022, shirika la Human Rights Watch (HRW), ilishutumu wakala wa mpaka wa Ulaya ‘Frontex’, kwa kuunga mkono vikosi vya Libya na ndege zisizo na rubani kuzuia boti za wahamiaji, na kwamba mipango hiyo ya mateso imekuwa ikifadhiliwa na Pesa za mataifa ya Ulaya.

Kenya: Wabunge wapya kutalii Bungeni
Masoud Djuma aomba radhi Dodoma Jiji FC