Wauguzi na Wakunga nchini, wametakiwa kuweka kipaumbele cha kuwahudumia watoto wenye ulemavu na kuwaunganisha mapema sehemu husika za kupata huduma za afya mara wanapogundulika, kwani hatua hiyo inaweza kupunguza ukubwa wa tatizo la ulemavu.

Rai hiyo, imetolewa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI Amina Mfaki  wakati akifunga mkutano wa Wauguzi na Wakunga Viongozi  ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Kaimu  Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI  Bi.Amina Mfaki  akizungumza katika ufungaji wa mkutano wa Wauguzi na Wakunga Viongozi  ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Amesema, endapo uchunguzi ukibaini mapema tatizo la ulemavu na huduma stahiki zikamfikia kwa wakati tatizo linaweza kupungua, hivyo ni wajibu wa kila Mkunga na Muuguzi kutoa taarifa mapema na kumuunganisha mtoto katika ngazi za juu mara tu anapozaliwa na kugundulika kuwa ni mlemavu.

Ulemavu unatokana na vyanzo mbalimbali, wakati mwingine kabla ya mtoto hajazaliwa mama akiwa mjamzito, rai yangu kwa Wauguzi wanapotambua mapema ulemavu waweze kumuunganisha mtoto huyo na huduma stahiki hii itasaidia mtoto kuweza kuhudumiwa kwa haraka na kupunguza ulemavu alionao au kumaliza kabisa,” amesema Amina.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya  Ziada Sellah akionesha tuzo aliyopatiwa kwa utendaji mzuri wa kazi.

Awali, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya  Ziada Sellah amesema  mkutano huo umeenda sambamba na uzinduzi wa mwongozo unaohimiza utoaji wa huduma za afya zinazojali utu na zenye staha hivyo akatoa wito kwa Wauguzi kote nchini kutoa huduma zenye heshima na upendo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wauguzi wakuu wa Mikoa  Alhaj Ahmed Chibwana amesema katika mkutano huo wa Wauguzi na Wakunga Viongozi wametoka na maazimio mbalimbali ikiwemo maazimio ya kuweka mkakati wa pamoja wa kupunguza vifo vya Mama na Mtoto.

Chuo Ustawi wa jamii chawafunda Wadada wa kazi majumbani
Tafsiri maboresho sheria ya madini, GGML ni mfano: Dkt. Kiruswa