Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeamua kuitoa nje ya hifadhi ranchi ya Usangu kwa ajili ya shughuli za ufugaji wa kisasa
Majaliwa ameyasema hayo, wakati akizungumza na wadau, wawekezaji wa Bonde la Usangu, wakulima wa mpunga, wamiliki wa mashine za kukoboa mpunga na wafugaji Januari 16, 2023 Mkoani Mbeya.
Amesema, “GN namba 28 iliingiza ranchi ndani ya hifadhi, lakini ili wafugaji wawe huru tumeindoa na hivyo itakuwa nje, tumeacha na mito kadhaa ambayo itahifadhiwa kwa sheria za mazingira.”
Hata hivyo, Majaliwa amewataka wafugaji kujiamini kwani mifugo ni uchumi na kuongeza kuwa, “Tunataka tuondokane na uchungaji na kuwafanya Watanzania wafugaji kuacha kutembea umbali mrefu na ng’ombe kwani inaondoa thamani ya nyama, tunataka mfuge kisasa.”