Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Gabriel Jesus amewatumia salamu Mashabiki wa Klabu ya Arsenal, kwa kuonesha picha zake hadharani akiwa katika mazoezi mepesi kabla ya kurejea Dimbani.

Mshambuliaji huyo amekuwa nje ya Uwanja kwa majuma manne sasa, baada ya kuumia akiwa na kikosi cha Brazil wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2022, zilizounguruma nchini Qatar.

Jesus alikumbwa na majeraha ya mguu wakati wa mchezo wa Hatua ya Makundi dhidi ya Cameroon, uliomalizika kwa Brazil kupoteza kwa 1-0.

Hata hivyo bado haijaelezwa kwa kina Mshambuliaji huyo atarejea lini kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal, ambacho kwa sasa kinafanya vizuri katika Ligi Kuu ya England.

IS wakiri kuhusika na shambulio lililouwa watu 14 Kanisani
Tabasamu, tumaini jipya kwa wafugaji wa kisasa