Mamlaka za usalama katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, inamshikilia raia mmoja wa Kenya Abdirizak Muktar Garad (29), anayeshukiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi lililopigwa marufuku nchini Uganda, Allied Democratic Forces (ADF).

Mtu huyo inasemekana alipanga shambulizi la Jumapili kwenye kanisa lililoko Kivu Kaskazini ambapo watu 10 waliuwawa na alikamatwa siku ya Jumapili, Januari 15, 2022 ambapo Kitengo cha Polisi Kenya kinachopambana na ugaidi (ATPU) kimemtambua mtu huyo kuwa ni mkazi wa kaunti ya Wajir, iliyopo kaskazini mwa Kenya.

Kanisa lililoshambuliwa nchini DRC. Picha ya Xinhua.

Msemaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC), Anthony Mualushayi amesema, tukio hilo la Kasindi, lililofanyika eneo la Kivu Kaskazini karibu na mpaka wa Uganda lilisababisha takriban watu 39.

Hakuna kundi lolote la kigaidi lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini jeshi la Kongo linawatuhumu kundi ADF, ambalo lilishambulia vijiji kadhaa na inadaiwa magaidi hao wanatokea nchini Uganda na hufanyia operesheni zao Kivu Kaskazini na Ituri mashariki mwa DRC.

Azam FC yazitangazia vita Simba SC, Young Africans
Kocha Nabi awakataa Fei Toto, Morrison