Serikali kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, imetuma salamu za pongezi kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz, Nandy pamoja na Zuchu.

Katika tuzo hizo mashuhuri za muziki za muziki Duniani za ‘All Africa Music Awards'(AFRIMMA), zilizotangazwa usiku wa kuamkia Novemba 16, 2020 jijini Dallas, Texas, Marekani, Mwanamuziki Nassib Abdul maarufuDiamond Platinumz alishindwa tuzo kwa kuwa msanii bora wa kiume Afrika Mashariki ambapo Msanii Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy alishinda tuzo ya kuwa Msanii bora wa kike Afrika mashariki na Msanii Zuhura Kopa maarufu Zuchu alitunukiwa tuzo ya kuwa msanii bora anayechipukia Afrika.

Neymar aingia kwenye kampeni za Victor Font
Ntibazonkiza: Simba SC walitaka niikache Young Africans

Comments

comments