Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, imesema imefanya maboresho katika mfumo mzima wa utunzaji kumbukumbu za ardhi, utozaji wa kodi na utoaji wa huduma za Sekta ya Ardhi ambapo zaidi ya jumbe 84,000 za simu zimetumwa kwa wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maboresho yaliyofanyika kuhusu ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.

Amesema maboresho yaliyofanyika kwenye mifumo unaowezesha wamiliki wa ardhi kupokea ujumbe kupitia simu za mkononi ambapo katika msamaha wa kodi ya ardhi uliotolewa na Rais Samia baadhi ya wananchi walishindwa kunufaika ikiwemo taratibu zinazowataka kufika katika ofisi za ardhi ili kukadiria na kujua deni la msingi na riba itakayosamehewa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula.

“Miongoni mwa maboresha makubwa yaliyofanyika katika kipindi hiki kifupi ni kuboresha mifumo ili iweze kutuma ujumbe mfupi wa maandishi unatumwa kwa wadaiwa wote kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati kupitia simu za viganjani,” amesema Dkt. Mabula.

Hata hivyo, zoezi hilo kwa Mkoa wa Dar es Salaam linaendelea na hadi kufikia Aprili 30, 2023 wamiliki wa ardhi katika Mikoa yote ya Tanzania Bara watakuwa wametumiwa jumbe kupitia simu za mkononi kuhusiana na madai ya kodi ya pango la ardhi.

Kifo: Cobra agomea busu la Selfie, kijana afariki kwa sumu
Serikali kushirikiana na taasisi ufanikishaji wanaoenda Hijja