Siku mbili baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kueleza kuwa amenunua ndege binafsi nchini Marekani kwa lengo la kueneza injili nchini, Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imetolea ufafanuzi taarifa hiyo.

Askofu Gwajima alisema kuwa amenunua ndege aina ya Gulfstream N60983 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.64. Aliweka kipande cha video kwenye mtandao wa Instagram akionesha kuifanyia majaribio katika viwanja kadhaa nchini Marekani.

I had a fruitful meeting with my friend Pastor Yohana Maginga in a Private Jet, Birmingham, Alabama, USA!

A post shared by Bishop Josephat Gwajima PhD ? (@bishopgwajima) on


Hata hivyo, Afisa Habari wa TCAA, Ali Changwila amesema kuwa Mamlaka hiyo haijapata taarifa zozote kuhusu ununuzi wa ndege. Aliongeza kuwa moja kati ya taratibu za awali za ununuzi wa ndege binafsi ni kuitaarifu Mamlaka hiyo ambayo hutuma wataalam wake kuifanyia ukaguzi na kujiridhisha kabla ya kutoa kibali.

Alisema ukaguzi huo huhakikisha kama ndege husika inakidhi vigezo vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

“Je, imekidhi vigezo vya ICAO? Inacho cheti cha kusajiliwa? Historia yake ikoje? Imekwisha muda wake? Imeshakatazwa kusafiri? Maana kuna ndege zimekwisha muda wa kutumika halafu zinauzwa,” Changwila anakaririwa na Mwananchi.

Askofu Gwajima yuko nchini Marekani katika sehemu ya ziara yake ya kikazi akihubiri injili na kufanya maombezi.

 

Eminem kuangusha 'mzigo mzito' mwaka huu, kumfukuzia Jay Z
Tabora yajipanga kuzitumia fursa Bomba la mafuta