Uongozi wa mkoa wa Tabora umesema kuwa umejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa unatoa elimu ya kutosha kwa vijana ili kuwawezesha kuchangamkia kila fursa zitakazojitokeza wakati wa ujenziwa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi  Tanga nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa mapema na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mradi huo ni fursa kwa wananchi wa Tabora.

“Tunataka tuwaelimishe na kuwahamasisha vijana, kinamama na wananchi wote wa mkoa wetu kuhakikisha wanazitumia fursa zote zitakazotokana na mradi huu ili waweze kujiendeleza na hii itasaidia kuinua uchumi katika jamii,”amesema Mwanri

 

Aidha, ameongeza kuwa jambo muhimu watakalolifanya ni kuhakikisha kuwa vijana wa Mkoani wa Tabora wanashirikiana kikamilifu na wataalamu ambao watakuwa wakijenga miundombinu ya mradi huo pamoja na kutoa huduma zitakazohitajika ili waweze kufaidika na fursa hiyo za mrai huo.

Hata hivyo, Mwanri amesema kuwa kwa uongozi na wananchi wa Tabora wanaona fahari kwa jambo kubwa kama hilo la kihistoria linafanyika katika Mkoa wao ambao bomba hilo litapitia katika Wilaya za Igunga na Nzega.

 

Serikali yazungumzia taarifa za Gwajima kununua ndege binafsi
Mtoto wa Chris Brown wa miaka mitatu aanzisha biashara kubwa