Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage amewataka wamiliki wote wa viwanda walioshindwa kuviendeleza, kuijsalimisha Ofisini kwake kabla ya Serikali haijachukua hatua kali dhidi yao.

Ameyasema hayo mapema hii leo mkoani Tanga walipotembelea kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Tanga Fresh, ambapo  amesema kuwa kamwe Serikali haiwezi kuwavumilia wawekezaji ambao wameshindwa kuendeleza viwanda hivyo.

Amesema kuwa Serikali ina nia thabiti ya kuleta mapinduzi ya viwanda nchini, hivyo katika suala hilo halitakuwa na mjadala wowote kwani atakachokifanya ni kuwanyang’anya na kuwagawia wale wenye uwezo wa kuviendesha viwanda hivyo.

“Kuanzia sasa nawaagiza wamiliki wote wa viwanda ambao wameshindwa kuviendeleza kujisalimisha ofisini kwangu mara moja, nawaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kuanza operesheni ya kukagua viwanda vyote kwenye mikoa yao,”amesema Mwijage

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ina mikakati mikubwa ya kuhakikisha inafikia malengo iliyojipangia ya kuibadili nchi kuwa Tanzania ya uchumi wa viwanda na wakati hivyo amesema hawatakuwa na mchezo katika hilo.

Wakenya wazidi kumiminika Tanzania, wahofia machafuko
Video: walioshindwa kuendeleza viwanda wanyang'anywe-JPM