Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah ameipongeza Benki ya NBC kwa kuendelea kutoa huduma bora za kifedha kwa wananchi wa Zanzibar na taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Abdulla aliyasema hayo wakati Akizungumza na viongozi wa benki ya hiyi alipokutana nao  katika ofisi ya Spika mjini Unguja, mara baada ya viongozi hao kuhudhuria kikao cha baraza la Wawakilishi wakiwa ni  wageni wa Spika wa Zanzibar, Mheshimiwa Ally Zubeir.

 “Nawapongeza sana NBC kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wa uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu wa Zanzibar. Endeleeni kuongeza wigo wenu wa kutolea huduma kwa kuongeza matawi na Mawakala ili muweze kuwafikia wananchi wengi zaidi. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawaahidi ushirikiano na kuendelea kuweka mazingira bora ya kufanyia biashara” alisema.

Kwa upande wake Spika wa Zanzibar, Mheshimiwa Ally Zubeiry, aliishukuru Benki ya hiyo kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo akitolea mfano misaada mbalimbali kwa jamii ambayo Benki hiyo imekuwa ikitoa kila mwaka. Spika Zubeiry alisifia pia udhamini wa Benki ya NBC katika ligi ya mpira wa miguu nchini, NBC Premier league kuwa ni wenye tija kwa taifa kwa kutoa vipato na kuibua vipaji.

Bondia aliyeonekana akirusha ngumi hewani afariki dunia
Rais Macron: Namuhitaji Zidane Ufaransa