Makali ya Sheria ya Mtandaoni yameanza kung’ata baada ya kesi saba kufunguliwa na kuwafikisha mahakamani zaidi ya watu 50 na wengine kufungwa tangu kutungwa na kuanza kutumika.

Kesi hizo ni pamoja na ile ya Mkurugenzi wa Jamii Forums, Mexence Melo, ambaye ni mmoja wa wanahabari waliokumbwa na nguvu ya sheria hiyo.

Hayo yamesemwa na na Mwanasheria wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Deogratias Bwire, wakati akiwasilisha  mada juu ya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni na Sheria ya Takwimu,amesema watu hao walikamatwa chini ya kifungu cha 16 kinachozungumzia kuchapisha na kusambaza taarifa au takwimu au habari kwa mfumo wa maneno au alama.

“Sheria hii inawabana sana watumiaji wa mitandao ya kijamii na waandishi wa habari, kifungu cha 32 kinalazimisha kuwasaidia polisi kutoa taarifa za wachangiaji wa mtandao wake kama Jamii Forums,”amesema Bwire.

Aidha, amesema kuwa kifungu cha 31 kinawapa polisi ruhusa ya mahakama ya kuchukua kompyuta za ofisi husika kwaajiri ya upelelezi kitu ambacho si sahihi.

 

 

Mbowe alaani kigogo wa chadema kufungwa
Video: Viongozi watatu wa Chadema wafungwa, Ujenzi wa hospitali wamng'oa kigogo