Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba Nchi ya Malawi, umepelekea shule za msingi na sekondari kuchelewa kufunguliwa kwa wiki mbili nchini humo kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Daily Nation, kimeeleza kuwa muhula mpya wa masomo ulipagwa kuanza Januari 3, kutokana na ongezeko la visa vya maambukizi ya kipindupindu na vifo serikali imelazimika kufuta mipango ya kufungua shule hivi karibuni.
Chapisho lilotolewa Desemba 22, 2022, Serikali ilisema kuwa kipindupindu kimeua watu 410 nchini Malawi tangu Februari huku 13,837 wakiwa wamepima ugonjwa huo, kati yao 338 walilazwa hospitalini.
“Kwa wanafunzi wengine wote katika wilaya zote za afya, mamlaka husika zinapaswa kuimarisha uzingatiaji wa hatua zilizopendekezwa za kudhibiti kipindupindu,” Jopo kazi la Rais wa nchi hiyo kuhusu Uviko-19 na kipindupindu lilisema katika taarifa.
Novemba 2022, Malawi ilipokea dozi milioni 2.9 za chanjo ya kipindupindu kutoka Umoja wa Mataifa wakati mlipuko huo ulipokuwa ukienea.
Malawi ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi barani Afrika, ina wakazi milioni 18 na wengi wao wanategemea kilimo cha kujikimu huku hali ya usalama wa chakula ikiwa ni mbaya kwa sababu ya athari za mabadiliko ya hali ya tabianchi.
Takribani wilaya 27 kati ya 29 za Malawi zimeathirika na mlipuko mkubwa zaidi kuripotiwa nchini humo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.