Mafanikio ya muziki wa msanii kutoka Nchini Nigeria Wizkid yanaendelea kupamba moto, hii inajidhihirisha kupitia namna ambavyo mapokezi ya kazi zake kuwa makubwa kutoka kwa Mashabiki wake kote Duniani.

Mafanikio hayo yakuja hasa katika kipindi hiki ambacho wimbo wake (Essence) aliomshirikisha @terms kuendeÄşea kuweka rekodi za kipekee kwenye charts mbali mbali kubwa za Muziki Duniani.

Mapema wiki hii Wizkid amefanya mahojiano maalumu na #Complex ambapo amezungumzia mambo mengi kuhusu safari ya maisha yake, Muziki nk, na moja ya mambo aliyoulizwa ni pamoja na mfanikio ya wimbo #Essence ambapo aliweka wazi  kuwa alijua kabisa wimbo huo ni mzuri na aliutoa bila ya kuwa na matarajio ya kuwa ungependwa na kuwavutia watu wengi Duniani.

“Nilijua kuwa #Essence ni wimbo mzuri, lakini huwa sitarajii mengi ninapotoa wimbo wangu wowote, huwa naachia tu nikitumaini kuwa watu wataupenda, nafikiri watu wanaupenda.” Alisema WizKid.

Mwamnyeto: Tulihimizwa kufanya kitu dakika 15 za mwanzo
Simba SC kuanza kuivutia kasi Jwaneng Galaxy