Baada ya kutupwa nje ya michuano ya mabingwa Afrika kwenye hatua za awali, mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka Tanzania bara, Simba leo watashuka dimbani kuminyana na maafande wa JKT Tanzania ili kusaka alama tatu ndani ya mzunguko wa ligi hiyo.
Simba wanatazamiwa kuutumia mchezo huo ili kuweza kurejesha furaha ya mashabiki wao ambao wanadaiwa kutofurahishwa kufuatia kutolewa mapema kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika na timu ya UD Songo ya Msumbiji kwa sare ya bao 1-1 na kuwapa fursa wapinzani wao kusonga mbele kutokana na bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kutoka suluhu.
Mchezo wa leo wa ligi huenda ukawa mgumu kwa Simba kutokana na kuhitaji kuanza msimu vyema pamoja na kuwafurahisha mashabiki wao ambao utapigwa kwenye dimba la Uhuru na ni wa kwanza kwao kwenye Ligi kuu soka Tanzania bara.
Katika michezo miwili ya msimu uliopita Simba iliweza kupata matokeo chanya kwa maafande hao baada ya mchezo wa kwanza kuinyuka JKT mabao 2-0 na raundi ya pili wakapata ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kuweka rekodi ya kushinda michezo yote ya ligi dhidi ya timu hiyo ambapo leo wanakibarua kigumu cha kuwakabili wekundu hao wa msimbazi.
- Anthony Joshua kujiuliza tena kwa Andy Ruiz Jr
- Serena Williams aubwaga ubigwa kwa chipukizi wa Canada
- Bajeti ya Simba msimu huu yawekwa hadharani