Wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameendelea kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Jana, wabunge hao walitoka kwa muda katika Ukumbi wa Pius Msekwa wakati naibu spika huyo alipokuwa akifungua semina kuhusu ubia kati ya sekta binafsi na umma (PPP) na walirejea muda mfupi baada ya kumaliza kusoma hotuba yake na kumwachia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Josephat Kandege kuongoza.

Hata hivyo, waliporejea walikaa upande mmoja wa ukumbi huo wakijitenga na wabunge wa CCM na baada ya kumaliza semina hiyo, wabunge hao walionekana wakikwepa kusalimiana na wenzao wa CCM.

Akizungumzia kitendo hicho, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema, “Wabunge wote wa Ukawa huwa tunaenda katika kamati, hilo hatujalikataa, tuliyokataa ni mambo ya michezo, ya kushiriki katika kantini, kusalimiana na vikao vyote vinavyoendeshwa na Dk Tulia,” alisema Mbatia

Serengeti Boys yaipigisha kwata Shelisheli Taifa
Waziri Nchemba Awaonya Polisi Matumizi ya Nguvu