Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa hapendi kutumia mtandao wa Twitter kama watu wanavyo mkosoa, lakini analazimika kufanya hivyo kwa kuwa hana imani na vyombo vya habari kwakuwa vimekuwa vikimshambulia kila kukicha.

“Nina mambo mengine ninayoweza kuyafanya, lakini siviamini kabisa vyombo vya habari, kabisa kabisa. Na hiyo ndiyo njia yangu pekee ya kuweza kujibu,” amesema Trump.

Tangu ashinde urais mwezi Novemba, bilionea huyo aliyewania kiti hicho kwa tiketi ya Republican amekuwa akitumia Twitter kutoa matamko ya kiutawala, akizungumzia sera za mambo ya nje na hata kumshambulia yeyote anayemuandama.

Mwishoni mwa wiki, bilionea huyo alishambuliwa vibaya mtandaoni baada ya kuhitalifiana na mtetezi wa haki za binadamu John Lewis kwa kauli zake za kibaguzi.

John Lewis, mtetezi wa haki za binadamu amesema kuwa hatahudhuria kuapishwa kwa Trump, sababu kubwa ikiwa ni uingiliaji kati wa Urusi kwenye uchaguzi.

 

Video: Viongozi watatu wa Chadema wafungwa, Ujenzi wa hospitali wamng'oa kigogo
Ratiba Ya Kombe La FA Yakaa Sawa