Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameahidi kuwa hatasita kutumia bomu la atomiki, ikiwa nchi yake itashambuliwa kwa bomu la nyuklia.

Taarifa ya Kiongozi huyo, imetolewa na vyombo vya habari vya serikali nchini humo ikiwa ni siku moja baada ya nchi hiyo kurusha kombora la masafa marefu ambalo viongozi mjini Tokyo wanasema lilianguka umbali wa kilometa 200 karibu na pwani ya Japan.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un. Picha ya Reuters.

Jana (Novemba 18, 2022), Marekani na Japan zilijibu hatua hiyo ya Korea Kaskazini kwa kufanya luteka ya kijeshi, ili kuonesha mshikamano baina ya mataifa hayo washirika, huku tishio la usalama katika eneo hilo likiongezeka.

Kim Jong Un, amekuwa akilaani luteka hizo za Marekani na kusema ni uchokozi hatua ambayo imetafsiriwa kuwa ni vuguvugu la kichinichini la kutaka kuanzisha mashambuliano.

Zaidi ya kodi na tozo 230 zimefutwa: Mpango
Watu Bil. 3.5 wanaugua magonjwa ya kinywa