Baada ya kupigwa nyundo ya kufungiwa kwa wimbo pamoja na video yake ya ‘Chura’ jana, Snura ameonesha hali tofauti na wengi walivyotarajia.

Mwimbaji huyo aliyetambulishwa kiuimbaji na wimbo wa ‘Majanga’ ametumia mtandao wa Instagram kueleza hisia zake lakini hakuwa na lolote linaloonesha amejutia ama ameshtushwa na uamuzi huo.

“Ingekua ndio hela leo ningekua bilionea lo!!! Nawapenda sana kwakweli na nawatakia usiku mwema,” Snura aliandika na kuipa sapoti kwa hastag “#utaipenda2_ndimuimekolea_malimao_kama__210_habarizetuwanazo_ilazaohatuna.”

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana ilitangaza sio tu kuufungia wimbo na video ya ‘Chura’, bali kumfungia pia msanii huyo kufanya matamasha ya wazi kutokana na wimbo wake kukiuka kwa maadili ya Tanzania. Serikali pia imetahadhari mtu yeyote kuhakikisha hasambazi video ya wimbo huo ili asikabiliwe na mkono wa sheria kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.

Snura pia ametakiwa kutoshiriki kwenye masuala ya muziki hadi atakapojisajili kwenye Baraza la Sanaa Tanzania.

Bondia Amir Khan Aahidi Kutumia Mbinu Mbadala
Rungu La FA Kuzishukia Spurs, Chelsea, Dembele