Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, amesema mlinda mlango namba moja wa kikosi chake David de Gea ndio bora kwa sasa, licha ya kukosolewa na wachambuzi wa soka barani Ulaya.

De Gea amekuwa akitupiwa lawama tangu ligi kuu ya England iliporejea, baada ya kusimama kwa miezi mitatu kwa sababu ya ugonjwa Covid-19, ambapo nahodha na mchezaji wa zamani wa Manchester United Roy Keane amedai kiwango Mspaniola huyo kimeporomoka.

Keane alisema “Anaumwa kiasi cha kufa” kutokana na David de Gea kushindwa kuokoa shuti la Steven Bergwijin lililoipa uongozi Spurs kabla ya kipindi cha mapumziko.

Licha ya kukosolewa huko, bado Solskjaer amemkingia kifua na kusema ataendelea kumuamini kwa kumpa nafasi ya kusimama katika milingoti mitatu ya kikosi chake.

“Sidhani kama ni vibaya kama unafungwa mabao mawili kwenye michezo saba, mechi zenyewe ni dhidi ya Manchester City, Chelsea, Tottenham na Everton (goli la bahati mbaya)”.

“Lile shuti la siku ya Jumatatu ningeweza kuliokoa, lakini muda mwingine nadhani asingeweza, amekuwa akifanya sevu bora sana hapa, amekuwa akishinda mechi akiwa nasi. Bado naamini ni kipa bora duniani.” Alisema Solskjaer.

De Gea amekuwa akipata changamoto kubwa ya nafasi yake hata akiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, ambapo kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga amekuwa tishio kwa sasa.

Sakata la Morrison: Young Africans wasisitiza mkataba wa miaka miwili
Kesi za mauzo ya silaha na Rushwa zaendelea kumtesa Zuma kizimbani