Bunge la Marekani, limesema linatarajia kuanzisha uchunguzi wa kutokuwa na imani na Rais wa Taifa hilo, Joe Biden kutokana na kile kinachoonekana ni shinikizo la Rais wa zamani, Donald Trump na washirika wake.
Kupitia taarifa ya Spika wa Bunge la Nchi hiyo, Kevin McCathy amesema uchunguzi wa Bunge kwenye familia ya Biden umefichua tuhuma za ufisadi, unaohitaji uchunguzi wa kina, uwepo wa mutumizi mabaya ya madaraka na kuzuia uchunguzi.
Hata hivyo, Ikulu ya Marekani kupitia msemaji wake Ian Smith imesema, hatua hiyo ni siasa zenye msimamo mbaya kwani Wabunge wa repablikan wamekuwa wakimchunguza Rais Biden kwa miezi 9 bila kupata ushahidi.
Hakuna Rais wa Marekani aliyewahi kuondolewa Ikulu kupitia kura ya kutokuwa na Imani, ingawa Rais Richard Nixon aliwahi kujiuzulu wakati bunge lilipokuwa likijiandaa kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye mwaka 1974.