Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Daniel Levy ametangaza hadharani kuwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini England na klabu ya QPR, Charlie Austin.

Levy amesema kiasi cha paund million 15 kimetengwa rasmi kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo ambaye alionekana kuwa mustakabali mzuri wa kuitetea QPR, lakini mambo yaliwaendea kombo na kujikuta wakishuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita.

Kiongozi huyo amebainisha kwamba lengo la usajili wa Charlie Austin, ni kuziba pengo ambalo linaachwa wazi na mshambuliaji kutoka nchini Togo, Emmanuel Adebayor, ambaye yu njiani kuelekea Villa Park yalipo makao makuu ya klabu ya Aston Villa.

Hata hivyo imeanza kuhisiswa huenda kiasi cha paund million 15, kikakataliwa na uongozi wa QPR, ambao tayari umeshaonyesha msimamo wa kumuuza mshambuliaji wao kwa zaidi ya kiasi hicho cha pesa.

Uongozi wa QPR umeshaikataa ofa kama hiyo iliyowahi kutumwa na klabu ya Newcastle Utd, ambayo iliambatana na paund million 15 kwa lengo la kumsajili Charlie Austin.

Austin, aliifungia QPR mabao 18 katika ligi ya nchini England msimu uliopita, hatua ambayo ilimuwezesha kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.

CUF Wajipanga Kumjibu Ibrahim Lipumba, ‘Tumepitia Mengi’
Crystal Palace Wainasa Saini Ya Sako