Kitu kikubwa ambacho wasanii wengi hufurahi na kuona kwamba kazi zao zinaheshimiwa ni pale atakapohitaji ushirikiano wa kikazi kutoka kwa msanii mwingine na akafanikiwa kwa asilimia zote.

Rapper Stamina furaha yake imekamilishwa na Couple ambayo inafanya vizuri katika kiwanda cha muziki Jux pamoja na Vanessa Mdee baada ya kukubaliwa ombi lake la kufanya kollabo na Mwanadada huyo ambaye anafanya vizuri katika soko la Afrika..

Jumaaaaaaaaaaa

Kuna kipindi rapper Stamina alisikika kusema kuwa atafanya kazi na Vanessa lakini imekuwa kimya sana toka kutangaza hivo, Stamina amefunguka na kusema tayari kazi hiyo imefanyika anachosubiri kwa sasa ni kuangalia kipindi kizuri cha kuachia kazi hiyo.

”Ukweli kuhusu collabo na Vanessa Mdee nimeshafanya nasubiri tu muda wa kuitoa na lazima nitaitoa nasubiri wakati ufike, Vanessa ni msanii mkubwa Afrika kukubali kufanya collabo na mimi ina maana ametambua uwezo wangu, pia nimshukuru Jux ambaye ni muanzilishi wa hii project”. Stamina aliiambia Ayo Tv.

Jux na Stamina walishawahi kufanya wimbo wa pamoja ¬†uliokwenda kwa jina la ‘Alisema’ na hivi sasa ameshiriki kumuandikia mpenzi wake mashairi ya kiitikio kwenye wimbo ambao ameshirikishwa na Stamina.

 

 

Picha 5 kutoka Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM Dodoma
Video: 'Jeshi la Polisi halikutenda haki kupiga marufuku mikutano ya Vyama pinzani' - LHRC