Muigizaji maaarufu Steven Nyerere amefunguka kuhusu wasanii kurekodi video za faragha na kuziweka katika mitandao ya kijamii na kuomba baraza la sanaa ”BASATA” na vyombo vya ulinzi kutoa mfano ili kujenga kizazi kilichopo.
Ni baada ya video ya faragha ya muigizaji wa bongo movie Menina Attick kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza na dar24 media msanii huyo amesema kuwa Menina anamakosa hakusataili kufanya kitu alichokifanya kwa sababu ni mtu mzima alikuwa anajua linalofanyika, sheria ifuate mkondo wake.
Ameongeza kuwa kuna wasanii ambao wamevamia kwenye sanaa ndio hawa wanaofanya vitu vya hovyohovyo na kufanya sanaa ya bongo movie iendelee kushuka na kuendelea kuzorota, na ambapo ameomba watuhumiwa wapewe adhabu ya miaka miwili jela.
”Watanzania tusiwe wepesi kuhukumu watu lakini pia tusiwe wepesi kutetea watu kabla hatujajua nini kinachoendelea watu wengi wanajitokeza polepole jamani mtu mzima pole ya nini? tunahurumia tu kama kijana umri wake unanafasi ya kufanya mambo makubwa lakini unapofanya mabo ya hovyohovyo unakatisha ndoto yako” amesema steve
Naye msanii wa bongo fleva Baraka the prince amefunguka suala la kujirekodi video na picha akiwa na mpenzi wake Naj Dattani.
“Haiwezi ikatokea hicho kitu, hata tukiwa tumeeachana kwa sababu mimi na yeye hatujawahi kuwa na mazoea hayo, halafu Najma namchukulia kama mke wangu, sina ujasiri wa kumuomba tujirekodi picha au video zisizo na maadili, siku zote mwanaume anayejitambua na anayejiheshimu hawezi kumuomba mpenzi wake mjirekodi wakati mkiwa faragha”amesema Baraka.
Baraka ameongeza kuwa mwanaume ndiye huanza kuomba kujirekodi ila mwanamke hawezi kufanya hivyo hata siku moja, kwa hiyo ukifanya kitu kama hicho, unamchukulia mpenzi wako.