Eric Maxim Choupo-Moting alifunga mabao mawili katika mchezo ambao Stoke City ilizima mbio za ushindi mfurulizo walioanza nao Manchester United baada ya kuilalazimisha suluhu ya mabao 2-2.

Dakika ya 43 mshambuliaji Choupo-Moting aliipatia bao la kuongoza Stoke City kabla ya Paul Pogba kupiga mpira  kichwa uliomgonga Marcus Rashford begani na kutinga wavuni nakufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sale ya 1-1.

Kipindi cha pili Romelu Lukaku aliiweka mbele Man United kwa kufunga bao la pili lakini mshambuliaji mpya wa Stoke Choupo-Moting alisawazisha bao hilo katika dakika ya 63.

Jose Mourinho alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Marcos Rashford na Herrera na Juan Mata na Anthony Martial lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwani mpaka firimbi ya mwaisho ina pulizwa mchezo huo ulimalizika kwa sale ya 1-1.

Kwa matokeo hayo bado Manchester United wanabaki kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wamevuna pointi 10 baada ya kucheza michezo minne, wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa na mahasimu wao Man City amabo pia wana pointi 10 wakiwa nafasi ya pili.

Hakukuwa na kupeana mikono kati ya kocha wa Manchester United Jose Morinho na kocha wa Stoke City Mark Hughes baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

 

Wapiga dili wa madini wawekwa kikaangoni
Lissu anena baada kupata fahamu