Serikali imetoa mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa Taifa na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, ambapo inatarajia kukusanya na kutumia Sh. trilioni 34.88, ambazo kwa kiasi kikubwa zitatumika kwenye miradi ya ujenzi na uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu.

Akiwasilisha mapendekezo mbele ya wabunge jana,  Waziri wa fedha na mipango, dkt. Philip Mpango amesema kwa kuzingatia sera za bajeti kwa mwaka 2020/21 sh. trilioni 34.88 zinatarajiwa kukusanya na kutumika.

” Mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti ya mwaka 2020/21 yamezingatia mahitaji halisi ya ugharamiaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, ulipaji wa mishahara, deni la serikali pamoja na vipaombele vingine vya taifa” amesema dkt. mpango.

Amesema ” Bajeti ya maendeleo inajumuisha sh trilioni 10.16 fedha za ndani, sawa na asilimia 78.8 na trilioni 2.74 fedha za nje. matumizi haya yanajumuisha gharama za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020″

Na kufafanua kuwa ” Mapendekezo ya kiwango na ukomo yanajumuisha mapato ya ndani ya sh trilioni 24,07 sawa na asilimia 69 ya bajeti yote, mikopo ya ndani trilioni 4.9, mikopo ya nje yanye masharti ya kibiashara trilioni 3.04 na misaada ya mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo trilioni 2.8 sawa na asilimia 8.2 ya bajeti yote.

Mpango amesema bajeti ya mwaka 2020/21 ni ya mwisho katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015, hivyo bajeti hiyo itaendelea na utekelezaji wa maeneo makuu manne yaliyoainishwa katika ilani ambayo ni kuondoa umasikini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Mfanyakazi auawa kwa tuhuma za kuiba elfu 50
Watanzania wachomwa moto kwa imani za kishirikina Zambia