Imetokea hali ya sintofahamu ya watu watano wa familia moja wanaosadikika kufa kwa ugonjwa wa ebola na wengine wawili kuchunguzwa eneo la Maruku Bukoba Vijijini Mkoani Kagera.

Kufuatia taharuki hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amekutana na Waandishi wa Habari na kuzungumzia tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila.

Amesema, “inasemekana kuna watu ambao wamefariki na Serikali ya Mkoa kushirikiana na Wataalam wa Afya kupata meseji hizo, tumewasiliana na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na Mganga Mkuu wa mkoa kufanya njia za haraka kufika maeneo yanayotajwa, ili kufatilia kwa kina.”

Hata hivyo, Chalamila amesema tayari wamewasiliana na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa ajili ya kufuatilia jambo hilo ili kuweza kupata ukweli na taarifa zaidi zitatolewa.

Endelea kufuatilia kurasana za Dar24 Media kwa taarifa bila mipaka.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 17, 2023
Ushindi mara 36 dau la Kasino ya Mtandaoni Meridianbet