Serikali nchini China, imetoa taarifa za kufunga maeneo yenye mikusanyiko wa watu wengi kufuatia mlipuko mpya wa maapukizi ya virusi vya Corona, ambapo watu 57 wamebainika kuwa na maambukizi hayo.

Msemaji wa Serikali katika jiji la Beijing amewaambia raia kuwa kuna idadi kubwa ya watu waliobainika kuwa na Corona, hivyo kuamua kufunga maduka makubwa na maeneo ya mikusanyiko.

Hta hivyo Serikali ya China inanuia kuchukua hatua zaidi ndani ya saa 24 kudhibiti wimbi la pili la maambukizi ya virusi hivyo.

Maambukizi hayo ni makubwa kutangaza tangu China itangaze kuwa imedhibiti ugonjwa huo Aprili 2020. Idadi hiyo inafanya China kuwa na jumla ya maambukizi 83,123.

Mufti atangaza Madrasa za wanafunzi wakubwa kufunguliwa
Yaliyojiri simu ya Magufuli kwa Rais Mpya wa Burundi