Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida Mzalendo Widege amesema Taasisi hiyo imebaini kuwepo kwa mianya ya rushwa katika baadhi ya halmashauri ikiwemo ya mkalama kwa kukusanya michango kutoka kwa wananchi, kutumika kabla ya kuingizwa kwenye akounti za vijiji.

Widege akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari-Machi 2023alisema katika uchunguzi aliofanya amebaini fedha za michango zinztumika kabla ya kuingizwa kwenye akounti za vijiji na baadhi ya wanancchi hawapewi stakabadhi.

Aidha amesema kuwa wameibaini mianya ya rushwa katika usimamizi wa fedha za miradi ya maji chini ya kamati za maji za jumuiya za watumia maji ambapo wajumbe wa bodi wanajilipa posho kubwa hakuna muongozo wa viwango vya posho na mishahara na ukaguzi mahesabu haufanyiki.

Widege akizungumzia uendeshaji wa masoko katika Halmashauri ya wilaya ya manyoni amesema wamebaini hakuna sheria ndogo za Halmahsuri zinazosimamia uendeshaji wa masoko, kuna usimamizi hafifu wa soko na kupelekea vizimba kuwa wazi na wafanyabiashara wachache kulipa kodi.

Mambo mengine waliyobaini ni matumizi hayafuati utaratibu mafano ununuzi wa umeme na malipo ya mhudumu baadhi ya mapato hayaingizwi kwenye mfumo wa mapato kama mapato yatokananyo na maji na choo rejesta ya wafanyabiashara hazihusushwi na kuna malalamiko ya mpango wa uboreshaji wa soko.

Akizungumzia kuhusu uendeshaji na usimamizi wa vyama vya walimu Manispaa ya Singida amesema wamebaini walimu wanakatwa makato ya CWT bila ridhaa yao ba bila kujaza fomu ya TUF15 ukinzani wa maslahi mjumbe wa chama kuhusika katika nakala pale mwananchama anapotaka kujito.

Alitaja mambo mengine waliyobaini ni kuwepo kwa mkataba wa uwakala baina ya manispaa ya Singida na chama chenye wanachama wengi ambayo haijapitishwa kwa muda mrefu (kuhuisha), mwajiri kukata fedha ya uwakala kwa wanachama na kuwasilisha CWT bila kuwa na akounti maalumu.

Mamia waandamana kuipinga Serikali
Afikishwa Mahakamani kwa kujifanya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa