Shirika la Umeme nchini (TANESCO), ambalo hapo awali liliwataarifu wateja wake kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzi data ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wa malipo ya kabla (LUKU), na kuwataarifu kuhusu kushindwa kununua umeme kwa muda wa siku nne limesitisha mpango huo.

TANESCO ilisema, kuanzia siku ya Jumatatu Agosti 22 hadi 25, 2022, muda wa saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi watasitisha zoezi hilo, ambapo sasa taarifa iliyotolewa leo Agosti 17, 2022 na Kurugenzi ya Mawasiliano na Masuala ya Umma TANESCO makao makuu jijini Dodoma, imesema imesitisha zoezi hilo.

Taarifa hiyo, pia imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na kusema litatoa taarifa endapo mpango huo utapangwa kufanyika tena.

Awali, TANESCO ilitoa tangazo la kuwataarifu wateja wake kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzi data ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wa malipo ya kabla (LUKU), na kusema watakosa huduma hiyo kwa siku nne.

Ajenda ya Usalama na Biashara zatawala mkutano SADC
Zaidi ya Watoto 150 wafariki nchini Zimbabwe