Serikali nchini, kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Tanzania itaendelea kushirikiana na
Serikali ya Norway katika masuala ya maendeleo na hususan ufadhili wa miradi ya uhifadhi wa
mazingira na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati wa kikao cha majadiliano ya ushirikiano baina Serikali hizo mbili kilicholenga mikakati ya utekelezaji wa miradi ya uhifadhi wa mazingira na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Sehemu ya wajumbe wa Ofisi ya Makamu wa Rais na wa Ubalozi wa Norway wakifuatilia kikao cha majadiliano ya ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania na Norway kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma Machi 21, 2023.

Amesema Serikali ya Norway imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania katika sekta mbalimbali na kuongeza kuwa kwa sasa masuala ya mazingira yanazidi kupewa kipaumbele katika ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Aidha, Dkt. Komba ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana Norway katika masuala ya
usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali zinazopatikana baharini bila kuathiri hifadhi ya mazingira na kuanisha hatua mbalimbali zilizofikiwa katika juhudi za uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

Uchafuzi wa Mazingira: Serikali kukabili tabia za Binadamu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 22, 2023